Features Nyimbo Za Kristo
Nyimbo za Kristo ni programu inayojumuisha mkusanyiko wa nyimbo 220 kutoka katika kitabu cha Nyimbo za Kristo cha kanisa la Waadventista Wasabato kwa lugha ya Kiswahili kama kilivyohaririwa na kuchapwa na TANZANIA ADVENTIST PRESS (TAP).Programu hii imeandaliwa kukuwezesha kumwamudu Mungu kwa njia ya uimbaji mahali popote na muda wowote, Nyimbo za kuburudisha, kutia moyo na kukufariji wakati wa huzuni.
Sifa za program ni kama zifuatazo:-• Inahusisha eneo la utafutaji ambapo unaweza kutafuta wimbo kwa namba au kwa neno unalokumbuka liwe jina la wimbo kwa Kiswahili, kwa kiingereza au maneno yaliyo ndani ya wimbo.• Inakuwezesha kuweka nyimbo unazozipenda katika orodha tofauti na hivyo kuupata kwa urahisi wakati mwingine, pia unaweza kuuondoa pale unapoona inafaa.• Inakuwezesha kuona nyimbo kwa makundi.• Inakuwezesha kufuatilia wimbo kwa njia ya ala za sauti (thanks to hymnserve.com for the accompaniments).• Inakuwezesha kucheza ala ya wimbo hata usipokuwa kwenye programu• Inakuwezesha kuona wimbo unaocheza• Inakuwezesha kukuza ukubwa wa maandishi wa maneno ya wimbo kadri unavyoona inafaa.• Inakuwezesha kuona wimbo uliofunguliwa mara ya mwisho kwa kuuangaza.• Inakuwezesha kushiriki maneno ya wimbo na ndugu jamaa na marafiki kwa urahisi.• Inakuwezesha kubadili muonekano wa programu unaofaa katika mazingira ya Mwanga au Giza ili kuwezesha uono usioumiza macho.
Programu hii imeandaliwa na kutengenezwa na Justin Diva na Godfrey Diva kwa utukufu wa Mungu.
Secure & Private
Your data is protected with industry-leading security protocols.
24/7 Support
Our dedicated support team is always ready to help you.
Personalization
Customize the app to match your preferences and workflow.
See the Nyimbo Za Kristo in Action
Get the App Today
Available for Android 8.0 and above